Thursday, November 30, 2017

Mawingu Tz

Tetesi: Straika Mtibwa Kuchukua Nafasi Ya Ngoma Yanga Sc..

UONGOZI wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, wameanza kumfuatilia kwa karibu straika wa Mtibwa Sugar, Stahimili Mbonde, kwa lengo la kuongeza nguvu kwenye kikosi chao.
Mbonde, ambaye ameonekana kuwa lulu kwenye kikosi chake cha Mtibwa Sugar, huenda akamalizana na mabingwa hao watetezi endapo uongozi wa pande zote mbili utafikia makubaliano.
Kocha wa Mtibwa, Zubery Katwila, alisema kwamba yeye hana tatizo kama mchezaji huyo atakwenda Yanga, kwa sababu wao hawana tabia ya kumng’ang’ania mchezaji kwa sababu wana uwezo wa kuzalisha wachezaji wapya na huo umekuwa ni utamaduni wao
kama klabu.

“Hiki ni kipindi cha usajili, vitu kama
hivyo havikwepeki, ni taratibu tu kufuatwa, ingawa Mbonde bado ni mchezaji mzuri ambaye anaweza kutusaidia katika mechi za ligi
kuu msimu huu. Ila ikitokea kwamba Yanga wanahitaji kumsajili tutamruhusu bila matatizo, ingawa lazima taratibu zifuatwe,” alisema.

Straika huyo amekuwa msaada zaidi kwenye kikosi chake na amekuwa akikabiliana na mabeki wa timu pinzani na hata uchezaji wake umekuwa hautofautiani sana na ule wa mchezaji wa kimataifa, Donald Ngoma.

Tupe Maoni Yako