UONGOZI wa Klabu ya Simba umewapa wachezaji wake siku saba za kupumzika baada ya hapo wachezaji hao watarejea kwa ajili ya kujifua ili kujiandaa na mechi za ligi na michuano ile ya kimataifa.
Simba inaingia katika mapumziko hayo ikiwa ndiyo kinara katika msimamo wa ligi ikiwa na alama 23 baada ya kucheza michezo 11 na inatarajiwa kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Meneja wa klabu hiyo, Richard Robert alisema kwa sasa wametoa mapumziko kwa timu ili watakaporejea waanze kazi rasmi kujiwinda na michezo ijayo.
“Tumetoa mapumziko kwa wachezaji ya siku saba baada ya hapo watarejea ili kuweza kuendelea na mazoezi kama mnavyofahamu tuna michuano mbele yetu mikubwa ile ya ligi kuu na Kombe la Shirikisho.
“Tutaanza mazoezi na timu licha ya kwamba wengine watakuwa kwenye michuano ya Chalenji lakini tutaendelea mpaka wale watakapomaliza na watajiunga na timu na lengo ni kufanya vizuri kwa kujikita vizuri katika nafsi ya juu,” alisema Richard.
Tupe Maoni Yako