Showing posts with label SIMBA. Show all posts
Showing posts with label SIMBA. Show all posts

Friday, January 12, 2018

Mawingu Tz

Kisa Simba, Julio Ataka Nyumba Oysterbay

Kikosi cha timu ya Simba.
BAADA ya Simba kuonekana kusuasua ka­tika mechi za hivi karibu­ni, Kocha Mkuu wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amefun­guka kama timu hiyo itamuhi­taji yuko tayari kwenda kuwa kocha mkuu lakini atahitaji apewe nyumba ya kisasa eneo la Oysterbay.

Hii ni baada ya kuwepo taarifa kuwa Simba inahitaji huduma ya kocha huyo ambaye kwa sasa anainoa timu hiyo ya Ligi Daraja la Kwanza.

Julio alisema kuwa Simba kama kweli inamuhitaji inatakiwa kufuata yale ambayo anayahitaji yeye na siyo kinyume cha hapo.

“Simba wakitaka mimi nikafundishe timu yao sina tatizo lakini ni lazima wafuata yale ambayo nataka, kwanza wanipe ukocha mkuu, pili nyumba ya kisasa mae­neo ya Oysterbay, gari na hudumu zote ambazo wale makocha Wazungu wakija wanapewa.
“Pia wanapaswa kujua wakinipa hiyo kazi sitaki ku­ingiliwa kwenye kazi yangu mimi pamoja na benchi la ufundi kila watu watambue majukumu yao hapa ndipo timu inaweza kuwa na nafasi ya kufanya vizuri,” alisema Jamhuri.

Tuesday, January 9, 2018

Mawingu Tz

Alichosema Masoud Djuma Baada Ya Kina Mkude Na Kichuya Kutoonekana Benchi...


Alichosema Masoud Djuma baada ya kina Mkude na Kichuya kutoonekana Benchi baada ya kufanyiwa sub.
Jana story kubwa ilikuwa ni Simba kutolewa michuano ya Mapinduzi lakini story nyingine ikaibuka katikati yake kufuatia baadhi ya wachezaji wa Simba kutoonekana katika benchi mara baada ya kutolewa(Kufanyiwa sub) na badala yake kuonekana wamekaa maeneo mengine kabisa ya uwanja wakifatilia mechi.
Masoud Djuma msomaji  ni kocha msaidizi anayeiongoza Simba amewatetea kina Mkude na Kichuya kwa kusema kuwa yeye ndiye aliyewaruhusu wachezaji hao kuondoka katika benchi mara baada ya kuwafanyia mabadiliko.
Masoud amesema wachezaji hao walikuwa wamechoka na hivyo aliwaruhusu waende wakafanyiwe massage vyumbani na hakukuwa na ulazima kwa wao kurejea benchi na wala siyo Tatizo la Nidhamu kama ambavyo wengi walitafsiri.
Katika mchezo huo kati ya Simba na URA kutoka nchini Uganda Simba ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa wachezaji Shiza Kichuya, Nicolas Gyan, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin na Mwinyi Kazimoto na nafasi zao kuchukuliwa na Mo iBRAHIM, James Kotei, Yusuph Mlipili, Laudit Mavugo na Said Hamis Ndemla.
Simba katika mchezo huo alihitaji ushindi ili kujihakikishia kufuzu katika hatua ya nusu Fainali ya michuano hiyo ya Mapinduzi lakini aliishia kufungwa bao moja pekee bao likipatikana kipindi cha kwanza mara baada ya mchezaji Deboss Kalama kuwahadaa mabeki wa Simba na Kuachia Shuti kali lililomshinda kipa Emmanuel Mseja.
Nusu Fainali zitachezwa kesho Jumatano kati ya Yanga na URA na Azam na Singida United katika uwanja wa Amani Zanzibar.


Mawingu Tz

Niyonzima Arejesha Matumaini Simba

WAKATI wenzake wakiwa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi huko visiwani Zanzibar, kiungo mchezeshaji wa Simba, Mnyar­wanda, Haruna Niyonzima yeye yupo jijini Dar es Salaam akiendelea kujifua ufukweni.
Mnyarwanda huyo alibaki Dar ku­tokana na majeraha ya enka anayoen­delea kuyauguza yaliyomuweka nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili.
Kiungo huyo, alipata majeraha hayo akiwa kwenye mazoezi ya timu hiyo wakati kikosi hicho kikiwa na Mcam­eroon, Joseph Omog aliyesitishiwa mkataba wake hivi karibuni kabla ya msaidizi wake Mrundi, Masoud Djuma kukabidhiwa.
Akizungumza na Championi Ju­matatu, Niyonzima alisema ameanza programu hiyo ya kukimbia ufukweni kwa ajili ya kuiponyesha enka hiyo ili ipone kabisa.
Niyonzima alisema, wakati akien­delea na matibabu mengine atafanya mazoezi ya ufukweni kwani mchanga ni sehemu ya tiba kwa ajili ya jeraha hilo la enka linalomsumbua.
Aliongeza kuwa, hataki kuona akiendelea kusumbuka na jeraha hilo ambalo mara kwa mara linamtokea ili atakaporejea uwanjani lisijirudie.
“Mimi nipo Dar na sipo na timu Zan­zibar, kama unavyofahamu bado enka inanisumbua na hivi sasa nipo nafanya mazoezi ya kukimbia ufukweni huku nikiendelea kupata matibabu mengine hospitali.
“Na mazoezi haya ya ufukweni nayo ni sehemu ya tiba kwangu, kwani mchanga nao ni tiba kwa jeraha hili la enka inayonisumbua kwa muda mrefu,” alisema Niyonzima aliyetua kuichezea Simba katika msimu huu.
Mawingu Tz

Manara Alia Na Mapinduzi Cup Ashindwa Kujizuia, Atoa Mazito.

Baada ya klabu ya Simba kupokea kipigo cha pili katika michuano ya kombe la Mapinduzi kutoka kwa watoza Ushuru wa Uganda ( URA) Cha goli 1-0 Afisa habari wa klabu hiyo,Haji Manara amesema hana neno linaloweza kutosha kuelezea kilichotokea uwanjani.
Aidha amesema kuwa anayajua maumivu wanayopata mashabiki wa timu hiyo kwani yeye ni Msemaji lakini shabiki wa klabu hiyo.
“Kila sentesi niliyoandika nimefuta, hakuna neno linalotosha kuelezea hisia zangu kwa kilichotokea leo Amaan Stadium..nayajua maumivu ya wanasimba….shida yangu mimi ni msemaji kisha shabiki wa hii timu..najua sana pain yenu…but lazma maisha yasonge mbele…
🙏🙏
”>>>Manara


Mawingu Tz

Kisa Kipigo Cha URA, Omog Aivuruga Simba

Kung’olewa kwa Simba katika michuano ya Kombe la Mapunduzi baada ya kuchapwa bao 1-0, kumezua mjadala mpya kuhusiana na Kocha Joseph Omog.
Omog raia wa Cameroon, alifungashiwa virago vyake na uongozi wa Simba ambao ulitumia maneno matamu kusema wamekubaliana aondoke baada ya kuvuliwa ubingwa wa Kombe la Shirikisho na Green Worries inayoshiriki ligi daraja la pili. Lakini baada ya kipigo cha leo, mashabiki wameanza kuhoji kama ilikuwa sahihi kumuondoa Omog.
Baadhi ya mashabiki wa Simba na wa timu nyingine wameeleza kuwa Simba ilikurupuka kumuondoa kocha huyo. Lakini wako waliosema tatizo kubwa ni wachezaji wenyewe ambao wameshindwa kujituma na kuonyesha wanataka kushinda.
Pia kuna mashabiki ambao wameelekeza lawama zao moja kwa moja kwa Kocha Irambona Masoud Djuma kwamba mfumo wake unaonekana kuwa mgumu na si imara katika ulinzi.
Kipigo hicho leo kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar kimekuwa cha pili mfululizo kwa Simba. Mechi iliyopita, Simba ilikutana na kipigo kama hicho kutoka kwa Azam FC na matumaini yao kuendelea ilikuwa leo dhidi ya URA. Bao la URA lilipatikana dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza na kipindi chote cha pili, Simba ilishindwa kupata angalau bao moja.

Monday, January 8, 2018

Mawingu Tz

Masikini Aveva; Hali Yake Si Nzuri, Juhudi Zafanyika Kumhamishia Muhimbili Kwa Matibabu Zaidi


Masikini Mwenyekiti wa Simba! Maana hali ya afya ya Rais wa Simba, Evans Aveva bado siyo nzuri kwani jana jioni ndugu na marafiki wa karibu walikuwa kwenye mipango ya kumhamishia Hospitali ya Muhimbili.

Aveva jana alikimbizwa kwenye Hospitali ya Temeke, Dar baada ya hali yake kubadilika akiwa mahabusu kwenye Gereza la Keko.

Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, wanakabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za klabu hiyo na kutakatisha dola 300,000 (zaidi ya Sh 650 milioni) na wamekuwa rumande tangu Juni 29, mwaka jana.

Taarifa zinaeleza, familia na marafiki wa Aveva walikuwa na mazungumzo na Jeshi la Magereza kwa ajili ya kuomba uhamisho wa hospitali kutokana na aina ya matibabu anayoyapata Hospitali ya Temeke.

Mtoa taarifa huyo alisema, rais huyo anahitaji kupatiwa matibabu mazuri yatakayoendana na ugonjwa ambao ni siri ili apate nafuu arejee katika hali yake ya kawaida.

“Aveva jana (juzi) asubuhi hali yake ilibadilika na kusababisha akimbizwe kwenye Hospitali ya Temeke kwa ajili ya kupata matibabu ya afya yake.

“Lakini wakati akiendelea na matibabu Temeke, baadhi ya ndugu na marafiki wamejaribu kuliomba Jeshi la Magereza kwa ajili ya kupata ruhusa ya kumhamishia Hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kupata matibabu mazuri,” alisema mtoa taarifa huyo.


Alipotafutwa Kaimu Makamu wa Rais wa timu hiyo, Idd Kajuna kuzungumzia hilo, simu yake ya mkononi haikuwa ikipokelewa, lakini alipotafutwa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa timu hiyo, Hajji Manara kuzungumzia hIlo, alisema: “Mimi nipo Zanzibar sifahamu chochote kuhusiana na taarifa hizo, naomba waulize watu waliopo Dar.”

SOURCE: CHAMPIONI