Tuesday, January 9, 2018

Mawingu Tz

Alichosema Masoud Djuma Baada Ya Kina Mkude Na Kichuya Kutoonekana Benchi...


Alichosema Masoud Djuma baada ya kina Mkude na Kichuya kutoonekana Benchi baada ya kufanyiwa sub.
Jana story kubwa ilikuwa ni Simba kutolewa michuano ya Mapinduzi lakini story nyingine ikaibuka katikati yake kufuatia baadhi ya wachezaji wa Simba kutoonekana katika benchi mara baada ya kutolewa(Kufanyiwa sub) na badala yake kuonekana wamekaa maeneo mengine kabisa ya uwanja wakifatilia mechi.
Masoud Djuma msomaji  ni kocha msaidizi anayeiongoza Simba amewatetea kina Mkude na Kichuya kwa kusema kuwa yeye ndiye aliyewaruhusu wachezaji hao kuondoka katika benchi mara baada ya kuwafanyia mabadiliko.
Masoud amesema wachezaji hao walikuwa wamechoka na hivyo aliwaruhusu waende wakafanyiwe massage vyumbani na hakukuwa na ulazima kwa wao kurejea benchi na wala siyo Tatizo la Nidhamu kama ambavyo wengi walitafsiri.
Katika mchezo huo kati ya Simba na URA kutoka nchini Uganda Simba ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa wachezaji Shiza Kichuya, Nicolas Gyan, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin na Mwinyi Kazimoto na nafasi zao kuchukuliwa na Mo iBRAHIM, James Kotei, Yusuph Mlipili, Laudit Mavugo na Said Hamis Ndemla.
Simba katika mchezo huo alihitaji ushindi ili kujihakikishia kufuzu katika hatua ya nusu Fainali ya michuano hiyo ya Mapinduzi lakini aliishia kufungwa bao moja pekee bao likipatikana kipindi cha kwanza mara baada ya mchezaji Deboss Kalama kuwahadaa mabeki wa Simba na Kuachia Shuti kali lililomshinda kipa Emmanuel Mseja.
Nusu Fainali zitachezwa kesho Jumatano kati ya Yanga na URA na Azam na Singida United katika uwanja wa Amani Zanzibar.



Tupe Maoni Yako