BAADA ya Simba kuonekana kusuasua katika mechi za hivi karibuni, Kocha Mkuu wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amefunguka kama timu hiyo itamuhitaji yuko tayari kwenda kuwa kocha mkuu lakini atahitaji apewe nyumba ya kisasa eneo la Oysterbay.
Hii ni baada ya kuwepo taarifa kuwa Simba inahitaji huduma ya kocha huyo ambaye kwa sasa anainoa timu hiyo ya Ligi Daraja la Kwanza.
Julio alisema kuwa Simba kama kweli inamuhitaji inatakiwa kufuata yale ambayo anayahitaji yeye na siyo kinyume cha hapo.
“Simba wakitaka mimi nikafundishe timu yao sina tatizo lakini ni lazima wafuata yale ambayo nataka, kwanza wanipe ukocha mkuu, pili nyumba ya kisasa maeneo ya Oysterbay, gari na hudumu zote ambazo wale makocha Wazungu wakija wanapewa.
“Pia wanapaswa kujua wakinipa hiyo kazi sitaki kuingiliwa kwenye kazi yangu mimi pamoja na benchi la ufundi kila watu watambue majukumu yao hapa ndipo timu inaweza kuwa na nafasi ya kufanya vizuri,” alisema Jamhuri.
Tupe Maoni Yako