Monday, December 18, 2017

Mawingu Tz

Wanachama Yanga Wacharuka, Wamfungulia Mlango Mzee Akilimali Aiache Yanga

Ukisema kimenuka wala hautakuwa imekosea baada ya baadhi ya wanachama wa klabu ya Yanga kutaka kuona mwanachama maarufu wa klabu hiyo anatimuliwa.

Wanachama hao wameonyesha kuchoshwa na tabia ya Katibu wa Baraza la  Wazee wa Yanga Ibrahim Akilimali za kupinga mabadiliko ya klabu hiyo hivyo imewalazimu kutoa mapendekezo ya kumfuta uanachama.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Katibu Mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa alitangaza rasmi nia ya klabu hiyo kuanza mchakato wa kwenda katika mfumo wa hisa jambo ambalo baadae Akilimali alisikika akipinga mfumo huo na kuomba Yanga wamtake radhi.
Akilimali amekuwa akishikilia msimamo wake kutaka Yanga ibaki kama zamani na wao wanaona kama anawachelewesha.

Hivyo kutaka Akilimali atupiwe virago na kuiachia Yanga endelee na “maisha” yake.


Akizungumza ndani ya Makao Makuu ya Yanga Makamu  Mwenyekiti wa tawi la Uhuru  Kaisi Edwin alisema,wamekutana wenyeviti wote wa matawi na kukubaliana kuandika barua kwa uongozi huo ili wamfutie uanachama mzee Akilimali

Tupe Maoni Yako