Wednesday, December 27, 2017

Mawingu Tz

Wachezaji Wanne Watakaotua Man United Januari

Manchester United inafuatilia wachezaji wanne kuelekea dirisha la uhamisho la Januari, kwa mujibu wa vyanzo vya Uingereza
Yahoo! Sport, kimenukuliwa na Daily Star, kikidai kuwa Mashetani Wekundu wanataka kumsajili winga wa Monaco Thomas Lemar, Justin Kluivert wa Ajax, Christian Pulisic wa Borussia Dortmund na Malcom wa Bordeaux.
Habari hizo zimesema kuwa bosi wa Manchester United Jose Mourinho amepewa bajeti ya paundi milioni 80 kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake kwenye uhamisho wa Januari.
Manchester United inaweza kuanza mchakato wa kuwasajili wachezaji hao wiki zijazo kwenye dirisha la uhamisho wa Januari.
Thomas Lemar Saint-Etienne Monaco
Mashetani Wekundu watakuwa wakipambana kuimarisha kikosi chao katika dirisha la katikati ya msimu baada ya kuachwa pointi 13 nyuma na vinara wa ligi Manchester City katika mbio za Ligi ya Uingereza.
Christian Pulisic Borussia Dortmund
Manchester United wanajipanga kurejea kibaruani Ligi ya Uingereza siku ya Boxing Day watakapoikaribusha Burnley Old Trafford.
Mashetani Wekundu wanashuka dimbani wakiwa wamepania kurudi kwenye njia za ushindi baada ya kuruhusu goli la kusawazisha dakika za majeruhi katika sare ya 2-2 dhidi ya Leicester City Jumamosi usiku.
Manchester United wamemaliza nafasi ya sita pamoja na kutwaa taji la Europa msimu uliopita.

Tupe Maoni Yako