Wachezaji walioachwa Simba dirisha dogo 2017
Klabu ya Simba baada ya kuwasajili Antonio Dayo Domingues na Mghana Asante Kwasi ambaye aligeuka kuwa gumzo mitandaoni na kwenye vyombo vya habari baada ya kuwapo msuguano kati ya Lipuli (Timu yake) Simba na Singida United wapo pia walioachwa na Simba.
Taarifa za Uhakika msomaji wetu zinasema kuwa Simba wameamua kuachana na wachezaji wake watatu wa Kimataifa Laudit Mavugo kutoka Burundi, Nicolas Gyan kutoka nchini Ghana na Method Mwanjali kutoka nchini Zimbabwe.
Laudit Mavugo na Gyan wanaachwa kutokana na kushuka kiwango hivyo kuonekana wanakula mishahara ya bure tu wakati Mwanjali sababu ya Umri na majeraha ya mara kwa mara ikitajwa kuwa ni sababu.
Kwa Upande mwingine inasemekana Mzambia Jonas Sakuwaha baada ya mvutano wa muda mrefu uongozi umeamua kumsaini
Tupe Maoni Yako