Huku siku za dirisha dogo la usajili Tanzania BARA kuelekea Kuisha kocha msaidizi wa Simba Masoud Djuma ambaye ndiye yupo na kikosi cha Simba kwasasa mara baada ya kocha mkuu Mcameron Joseph Omog kwenda kwao baada ya ligi kusimama amemuelezea Straika Jonas Sakuhawa.
Akizungumza mara baada ya kumuona katika mchezo kati ya Simba na KMC mchezo wa kirafiki Masoud Djuma msomaji wa Kwataunit.com alisema
” Kwa upande wangu na benchi la ufundi sina tatizo na mchezaji huyu, hapo amecheza akiwa ametoka kwenye mapumziko hana mazoezi ya kutosha lakini mmemuona uwezo wake, anaweza kutimiza majukumu yake awapo uwanjani, nafikiri kilichobaki na kwa viongozi tu kumpa mkataba. “
Katika mchezo wa kirafiki kati ya Simba na KMC Simba walifanikiwa kushinda bao 3 kwa 1 huku Sakuhawa akitupia bao 1 huku mengine mawili yakifungwa na John Bocco
Tupe Maoni Yako