KOCHA Mkuu wa Singida United, Hans van Der Pluijm raia wa Uholanzi, ametamba kuendelea kuzifukuzia kwa ukaribu timu kongwe za Simba na Yanga mpaka mwisho wa msimu huu kwani nia yake ni kuona anaipa mafanikio katika msimu wake wa kwanza.
Mholanzi huyo ambaye msimu uliopita alikuwa akiinoa Yanga kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Mzambia, George Lwandamina, hivi sasa anakinoa kikosi cha Singida United kilichopanda daraja msimu huu.Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Simba inaongoza ikiwa na pointi 23 sawa na Azam, Yanga ni ya tatu na pointi zake 21, huku Singida ikiwa ya nne ikijikusanyia pointi 20.
“Hatupo mbali sana na kinara wa ligi, ukiangalia msimamo wametupita pointi tatu tu ambazo zinaweza kupatikana kwenye mechi moja kama tukishinda, sisi tupo wa nne tukipitwa na Yanga kwa pointi moja, hivyo tutaendelea kupambana hadi mwisho kuona tunafikia malengo yetu ya kumaliza nafasi mbili za juu,” alisema Pluijm.
Tupe Maoni Yako