Saturday, December 9, 2017

Mawingu Tz

Kocha Simba Aongeza Dozi Kuimaliza Ndanda Fc,Azungumzia Hali Ya Kikosi

[​IMG]
KOCHA msaidizi wa klabu ya Simba, masoud Djuma, amesema mazoezi wanayoyafanya kwa sasa yana lenga kuirudisha timu hiyo kwenye makali yake waliyoanza nayo msimu huu.Kocha huyo raia wa Burundi kwa sasa ndiye anayesimamia mazoezi ya timu hiyo baada ya kocha mkuu Joseph Omog kwenda mapumzikoni.
Simba ilianza kwa kasi msimu huu kwa kuanza na ushindi mnono wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting kabla ya mambo kuanza kuwa magumu.
Kocha Djuma, alisema pamoja na kuongoza ligi, bado kuna mambo lazima wayaweke sawa kabla ya kurejea kuanza tena mikikimikiki ya ligi kuu iliyosimama kwa muda kupisha michuano ya Chalenji inayofanyika nchini Kenya.
“Kuna vitu tunafanyia kazi kwenye mazoezi, tunataka kuona tunarudi kwenye ligi na nguvu mpya.., suala la kufunga mabao katika nafasi tunazozitengeneza tunalifanyia kazi.., tutarudi tukiwa na kasi,” alisema Djuma.
Alisema kuwa ameongeza muda wa kufanya mazoezi ili kuwapa pumzi na stamina wachezaji wake.
“Wale waliopo kwenye majukumu ya timu zao za taifa tunaamini huko walipo wanafanya mazoezi na hata mechi za Chalenji wanazocheza ni mazoezi tosha,” alisema Djuma.
Alisema kwa sasa wanafanya mazoezi kwa masaa mawili mpaka matatu.
Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 23 baada ya kucheza michezo 11 ikilingana na Azam wanaoshika nafasi pili baada ya kuizidi idadi ya magoli ya kufunga, Yanga wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 21.

Tupe Maoni Yako