Siku kadhaa baada ya Simba kumtangaza Bilionea Mohammed Dewji kama mshindi wa zabuni iliyotangazwa na kumfanya Mo kuwa mshindi wa umiliki wa Hisa asilimia 49 ndani ya klabu ya Simba , Uongozi wa Juu Yanga nao wazungumza kuelekea Mabadiliko.
Kaimu mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga ambaye ndiye mwenyekiti kikatiba kutokana na aliyekuwa mwenyekiti Yusuph Manji kujiuzulu amesema Yanga katiba yao inawaruhusu kufanya mabadiliko ya kuruhusu kampuni kuanzishwa ndani ya Yanga na Yanga kumiliki kampuni hiyo.
"KLABU YETU KWA MUJIBU WA KATIBA KLABU YETU INARUHUSU KUANZISHA KAMPUNI AMBAYO ITAMILIKIWA NA KLABU KWA MAANA WANACHAMA KWA ASILIMIA 51 NA WAWEKEZAJI WENGINE WENYE HISA KWA ASILIMIA 49 KWAHIYO NAFIKIRI SISI HATUTAKUWA NA MBIO NDEFU SANA."
Sanga amesema katiba yao imeeleza juu ya suala hilo na ni katiba ya toka mwaka 2010 na serikali imeshatoa mwongozo kwahiyo mapema Sana Sanga ameahidi atakaa na kamati ya utendaji kuridhia na kisha watakaa kujadili na kuunda kamati itakayoshugulikia mchakato mzima wa mabadiliko ndani ya Klabu hiyo.
Tupe Maoni Yako