Friday, December 15, 2017

Mawingu Tz

Iniesta Atoa Ya Moyoni Kuhusu Suala La Neymar Kwenda Real Madrid

Mshambuliaji  wa Paris Saint- Germain, Neymar.
KIUNGO mkongwe wa Barcelona, Andres Iniesta amesema hana hofu kuhusu Neymar kujiunga na Real Madrid lakini akakiri kuwa ikitokea hivyo haitampendeza kutokana na uhusiano wa Neymar na mastaa wengine wa Barcelona wakati alipokuwa akiichezea timu hiyo.

Iniesta amecheza na Neymar kwa miaka minne kabla ya mchezaji huyo kuondoka na kuhamia Paris Saint- Germain lakini kumekuwa na taarifa za kuwaniwa kwa ukaribu na Real Madrid.
Kiungo mkongwe wa Barcelona, Andres Iniesta.
“Chochote kinaweza kutokea kwenye soka, kuna mambo ambayo yalionekana ni vigumu kutokea na yakatokea, sitashangaa lakini haitapendeza kwa kuwa kwa kuwa ni mchezaji mzuri lakini sina hofu,” alisema Iniesta.

Tupe Maoni Yako