Tuesday, December 19, 2017

Mawingu Tz

Baada Ya Kuzushiwa Kifo, Manara Apokelewa Msibani Kwa Shangwe Kuu


Msemaji wa Simba, Haji Manara amekutana na wakati mgumu baada ya kuzushiwa kifo.

Baadhi ya watu wametupia mtandaoni wakielezea kuwa Manara amefariki dunia.

Hata hivyo, Manara amesema taarifa hizo ni uzushi mkubwa na alikwenda msibani na kupokelewa kwa shangwe kwa kuwa tayari watu walipata taarifa kwamba amefariki dunia.



"Jaman ndugu zangu toka Jana kuna habari znazagaa kuwa nimekufa. Kaka yangu anaitwa Ramadhan kitenge alinipigia Jana kuwa kaona fb," anaelelezea Manara.

"Ndugu zangu na mama yangu mzazi nao walipigiwa simu, nikapuuza. Lakini leo wakati nikijiandaa kwenda msibani kwa mwanachama wetu maarufu dada Fii kambi.

"Nikapigiwa cm nyingi za kutaka kujua hali na uhai wangu na kweli nilipofika msibani nimekuta vilio vya kina mama kuwa nimefariki.

"Kiukweli mm ni mzima wa afya, siumwi chochote na Alhamdulillah naendelea na shughuli zangu kama kawaida. Kufa tutakufa tu kwa ahadi yake Mungu, puuzeni uvumi wa mitandaoni," anasisitiza Manara

Tupe Maoni Yako