Wednesday, December 6, 2017

Mawingu Tz

Alichokisema Mzee Akilimali Baada Ya Simba Kupitisha Uwekezaji Wa Mo Dewji


Katibu wa Baraza la Wazee wa  Yanga, Ibrahim Akilimali ameibuka na kusema kuwa mashabiki wa Simba wamekuwa wakiwazomea kuwa wanaiga mabadiliko kwao jambo ambalo siyo kweli, huku akiwapongeza.

Mzee Akilimali ameyasema hayo baada ya  mfanyabiashara bilionea na mwanachama wa Simba, Mohammed Dewji ‘MO’   kutangazwa kuwa mwekezaji ndani ya timu hiyo kufuatia kushinda zabuni ambayo mchakato wake ulikuwa ukifanyika kwa miezi kadhaa nyuma.

Mzee Akilimali alisema kuwa anaumizwa na kitendo cha kuambiwa wanaiga  kufanya mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa timu yao kutoka kwa watani zao licha ya wao kuwa wa kwanza lakini wakashindwa kukamilisha.

“Kwanza nasikitika pia naumia kwa hiki ambacho kipo cha kutuambia sisi Yanga tunaiga walichokifanya wenzetu lakini watu wanatakiwa wafahamu kuwa Yanga ndiyo wa kwanza kuanzisha mambo haya tangu mwaka 2007 na mimi ndiyo nilizunguka nchini nzima na wajumbe 30 kuelimisha jambo hilo.
 “Sasa kutokana na migongano ya kimawazo na viongozi waliopita wa wengine kushindwa kuliendeleza kabla ya Yusufu Manji kuleta mpango wake  ambao binafsi sikuweza kukubaliana nao  ndiyo leo tunaambiwa hivi, nawapongeza wao kwa hatua waliopiga japo kwetu inasikitisha kwa kuwa ni kitu ambacho kimezungumziwa kwenye katiba yetu ya Yanga,” alisema Mzee Akilimali.


Tupe Maoni Yako