
KLABU Bingwa nchini Dar Es Salaam Young Africans wameanza usajili wa dirisha dogo kwa kumuongeza beki wa kati Fiston Kayembe Kanku ambaye ni raia wa DR CONGO kwa kumsaini miaka 2.
Kanku anajiunga na Yanga akitokea katika klabu ya Balende Fc ya huko huko kwao DR CONGO, Mchezaji huyo kabla ya kusajiiwa Yanga aliwahi kuja kufanya majaribio katika klabu hiyo na amewahi kucheza kwenye mchezo mmoja wa Kirafiki akiwa na jezi ya Yanga mchezo kati ya Yanga na KMC inayoshiriki ligi daraja la kwanza katika uwanja wa AZAM (Azam Complex)
Kupitia Ukurasa maalum wa Yanga wameandika
Fiston ‘Festo’ Kayembe Kanku amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na #mabingwamara27 @yangasc akitokea Balende Fc ya DR CONGO. pic.twitter.com/YlAuRRJCga— Young Africans SC (@yangasc1935) November 25, 2017
Tupe Maoni Yako