Beki wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand amesema anaamini uwepo wa straika mkongwe Zlatan Ibrahimovic ndani ya kikosi cha United inawezekana unachangia Romelu Lukaku kukosa mabao.
Lukaku amekuwa na ukame wa mabao katika mechi za hivi karibuni ambapo amefunga bao moja katika mechi 11 zilizopita huku akishindwa kufunga usiku wa jana wakati timu yake ikipata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Watford.
Awali, Lukaku alifunga mabao 10 katika mechi 11 za mwanzoni mwa msimu huu lakini ssa mambo yameanza kwenda ndivyo sivyo.
“Najua ataondoka katika hali hiyo, kuna na mchezaji mkubwa kama Zlatan Ibrahimovic nyuma yako ambaye anasubiri nafasi ni presha.
“Kichwani inaweza kuwa hali hiyo inamvuruga na ikawa ni kitu kigumu kupambana nacho,” alisema Ferdinand.
Tupe Maoni Yako