Showing posts with label Ligi Kuu Bongo. Show all posts
Showing posts with label Ligi Kuu Bongo. Show all posts

Thursday, January 11, 2018

Mawingu Tz

Rage Aipa Makavu Simba Na Awapa Ujumbe Huu Mzito Kuhusu Suala La Ubingwa Wa Ligi

Ismail Aden Rage.
ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, ameibuka na kusema kuwa, ndani ya klabu hiyo kuna tatizo na kama hawa­takuwa makini, basi kuna uwezekano hata ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu timu hiyo ikauokosa.

Rage ameyasema hayo kufuatia Simba, Jumatatu kuondoshwa kwenye Kombe la Mapinduzi, huku pia ikiwa imeshaondolewa kwenye Kombe la FA.

Rage amesema licha ya Simba kuwa vinara wa ligi kwa sasa, lakini kama viongozi, wachezaji na benchi la ufundi hawatakuwa na umoja, timu itavurugana zaidi na kushindwa kufikia malengo.
“Ukiangalia Simba ya msimu huu naona kama imerudia makosa ya Yanga waliyowahi kuyafanya huko nyuma, wamesajili wachezaji wengi bila ya kuangalia uhitaji wa timu zaidi ya kuangalia majina tu. Hili ni tatizo.

“Tatizo lingine ninaloliona ndani ya Simba mpaka kusababisha kufanya kwao vibaya ni kutokuwa na umoja baina ya wachezaji, benchi la ufundi na viongozi, wanatakiwa kukaa chini na kumaliza tofauti zao haraka kabla hatari zaidi haijatokea. Kugombana kumepitwa na wakati.

“Haiwezekani leo hii eti wachezaji wanafanyiwa mabadiliko halafu wanaondoka kwenye benchi, huu ni utovu wa nidhamu. Nawasihi wote kwa pamoja wakae chini wamalize tofauti zao wafanye kazi kwani wana kikosi kizuri lakini mambo madogomadogo kama hayo ndiyo yanawasumbua,” alisema Rage.

Saturday, January 6, 2018

Mawingu Tz

Mara Baada Ya JKT Ruvu Kubadili Jina, Masau Bwire Atoa Msimamo Wa Ruvu Shooting Kuhusiana na Swala Hilo…

Afisa habari wa klabu ya Ruvu shooting,Masau Bwire ametoa msimamo wa klabu hiyo baada ya maafande wenzao klabu ya JKT Ruvu kutangaza kubadili jina na kuse.a kuwa wao kwa sasa sio kama jeshi bali ni kampuni.
Bwire  amewatoa hofu wapenzi na wanachama wa klabu hiyo kwa kusema kuwa klabu hiyo kwa sasa imebadili utaratibu na kutoka Jeshini hadi kuwa Kampuni na tayari imekwishajilowa.
“Baadadaa ya JKT Ruvu kubadili jina na kutangaza kwamba ndiyo timu teule ya JKT nchi nzima wengi walihofu na kutaka kujua hatima ya timu yao pendwa, timu jeuri, yenye viwango na ubora, Ruvu Shooting.”
“Ruvu Shooting ilitoka zamani Jeshini na kwa sasa ni Kampuni, tayari imesajiliwa kama Kampuni kwa jina la Ruvu Shooting star Camp Ltd.
Taratibu zote zilifuatwa, Kamati ya ukaguzi ya TFF/Bodi ya ligi walipita kukagua na kujiridhisha.”
Taarifa hiyo ya Masau Bwire imetoka mara baada ya uongozi wa klabu ya JKT Ruvu kupitia kwa msemaji wake Constantine  kutoa taarifa ya kubadili jina na sasa inaitwa JKT TANZANIA.Taarifa kamili hii hapa…
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUBADILI JINA LA TIMU
TIMU YA JKT RUVU INAYOSHIRIKI LIGI DARAJA LA KWANZA KUNDI A MSIMU HUU, TIMU HIYO SASA ITAJULIKANA KWA JINA LA JKT TANZANIA SPORTS CLUB, NA NDIYO TIMU ILIYOPITISHWA KUMILILIKIWA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA NA MA MASKANI YAKE YATAENDELEA KUWA MAKAO MAKUU YA JESHI HILO MLALAKUWA KWA WAKATI HUU, MABABADILIKO HAYA YAMEKUJA BAADA BAADA YA KUPATA MAELEKEZO TOKA BODI YA LIGI KWA TAASISI KUMILIKI TIMU MOJA, TARATIBU ZOTE ZIMEFUATWA KATIKA KUTEKELEZA AGIZO HILI, UONGOZI WA JKT RUVU UNATOA SHUKRANI ZA DHATI KWA BODI YA LIGI NA TFF KWA USHIRIKIANO MKUBWA WALIOUTOA KUPITIA MAMLAKA/IDARA ZAKE WAKATI WA MCHAKATO MZIMA KUHUSU SWALA HILI MHIMU KWA USTAWI WA TAIFA LETU KUPITIA MPIRA WA MIGUU, MWENYEKITI WA JKT RUVU LUTENI KANALI HASSAN MABENA ALIKWISHA TOLEA UFAFANUZI WA KINA KUHUSU SWALA HILI KUPITIA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI,
USHIRIKI FDL
TIMU YA JKT TANZANIA S . C IPO KAMBINI NA INAENDELELEA NA MAZOEZI KATIKA UWANJA WA MEJA JENERALI MICHAEL ISAMUHYO -MBWENI JKT, CHINI YA KOCHA MKUU BAKARI SHIME, TAYARI KWA MCHEZO WAKE NA TIMU YA MVUVUMWA FC JANUARY 13.KATIKA UWANJA WA UHURU, MIPANGO NA MALENGO YA KOCHA MKUU BAKARI SHIME NI KUHAKIKISHA TIMU INASHINDA KATIKA MICHEZO YOTE ILIYOBAKI ILI KUTIMIZA MALENGO WALIOJIWEKEA, NA WACHEZAJI WOTE WALIOPO KAMBINI WAPO ARI KUBWA KUELEKEA MCHEZO HUO
AZAM FA CUP
PAMOJA NA USHIRIKI KATIKA LIGI DARAJA KWANZA TIMU PIA INA JUKUMU LA KUWEKA USHINDANI MKUBWA KATIKA MASHINDANO YA AZAM FA CUP, AMBAPO TIMU IMESONGA MBELE NA IMEPANGWA KUCHEZA NA POLISI DAR KATIKA HATUA INAYOFUATA, NDIYO MAANA KOCHA BAKARI SHIME AMEIANDAA TIMU YAKE KWA MASHINDANO YOTE MAWILI MDA WOWOTE, SIKU YOYOTE NA MAHALI POPOTE, PAMOJA NA KUWA NA USHINDANI MKUBWA SHIME AMEKIRI HIYO NI CHANGAMOTO KUBWA KATIKA KULETA MATOKEO CHANYA KWA UPANDE WA TIMU YAKE
HISTORIA YA TIMU
TIMU YA JKT TANZANIA SC, ILINZISHWA MWAKA 1970 KATIKA KAMBI YA JKT MGULANI DAR ES SALAAM, NA ILIJULIKANA KWA JINA LA JKT KABAMBE, MWAKA 1973 TIMU HIYO ILIHAMISHIWA KATIKA KIKOSI CHA RUVU JKT MKOANI PWANI, NA MWAKA 1975,TIMU HIYO ILIBADILISHWA JINA NA KUITWA JKT RUVU NA MWAKA 1999 TIMU YA JKT RUVU ILIHAMISHIWA MAKAO MAKUU YA JESHI LA KUJENGA TAIFA MLALAKUWA JIJINI DAR ES SALAAM, DESEMBA 12,2017,TIMU HIYO ILIBADILISHWA JINA NA KUITWA JKT TANZANIA SC NA TARATIBU ZA KUPELEKA TAARIFA ZA MAANDISHI ZILIANZA KUTEKELEZWA NA MAFANIKIO MAZURI YAMEPATIKANA KUFUATIA ZOEZI HILI, UONGOZI WA JKT RUVU UNAWATAKA WADAU MBALIMBALI KUYAPOKEA MABADILIKO HAYO YA KISHERIA KWA MIKONO MIWILI
TAARIFA HII IMEANDALIWA NA
AFISA MTEULE DARAJA LA PILI, COSTANTINE MASANJA, AFISA HABARI JKT TANZANIA SC

Tuesday, January 2, 2018

Mawingu Tz

Msikie Yule Straika Aliyewaliza Yanga Kirumba


YULE straika wa Mbao FC, Habibu Kiyombo, aliyewafanyia Yanga kitu mbaya katika mechi yao ya Jumapili Uwanja wa CCM Kirumba amesema , anatamani awe mchezaji bora wa muda wote kama walivyo wakali Muargentina Lionel Messi na Mreno Christian Ronaldo.
Kiyombo ambaye ndiye aliyewafunga Yanga mabao yote mawili jana Jumapili walipocheza mchezo wa ligi kuu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
“Niliwahi kuwafunga bao moja kwenye mechi yetu ya mwisho ya ligi kuu, kwa hiyo hata jana Jumapili, nilitamani kuwafunga, jambo ambalo nimelitekeleza. Nawashukuru wachezaji na kocha wetu ( Mrundi Ettiene Ndayiragije) kwa kukamilisha malengo yetu,”amesema Kiyombo.
“Natamani kuwa mchezaji bora wa muda wote, mfungaji bora na timu yangu ili iwe nafasi nzuri kama wanavyofanya Messi na Ronaldo kule kwao, natamani sana hivyo nitazidi kupambana hadi nifanikiwe."
Mshambuliaji huyo ambaye tayari amefunga mabao 12, ambayo ni pamoja na ya FA na ligi kuu amesema, bado ushindani ni mkali kwa nyota wengine wanaopambana kusaka kiatu cha mfungaji bora hivyo hatakata tamaa hadi mwisho wa Ligi.
Mawingu Tz

Mashabiki Wa Simba Bhana CHeki Walichokisema Kuhusu John Bocco

Unaweza kusema mashabiki wa soka hawana kauli moja baada ya baadhi yao kumsifia mshambuliaji wa Simba, John Bocco kuwa anajituma sana.

Baada ya Bocco kufunga mabao mawili wakati Simba ikiimaliza Ndanda FC kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara, mashabiki hasa wa Simba wanaonekana kufurahishwa na mwendo wa Bocco.
Katika mijadala ya makundi mbalimbali pia kupitia mtandao wa Instagram, mashabiki hao wa soka wameonyesha kufurahishwa na Bocco.

Wengi wameeleza pamoja na kufunga lakini amekuwa akicheza kwa juhudi kubwa na inapaswa kuwa mfano kwa wengine,
Lakini wako waliosema, Bocco anaonekana ana malengo hata kuliko wachezaji wengi wa kigeni kwa kuwa hataki kufeli.
Wakati wakimwagia sifa kibao, siku chache zilizpita, mashabiki walikuwa wakilalama kwamba Bocco anaonekana kutokuwa na msaada.


Mara kadhaa, hadi uwanjani walikuwa wakipiga kelele kutaka Bocco ataolewe, madai kwamba hana msaada.
Mawingu Tz

Asante Kwasi Nae Atoa Ya Moyoni Kuhusu Tshishimbi

Asante Kwasi.
BEKI mpya wa Simba, Asante Kwasi, raia wa Ghana, ameibuka na kusema kuwa, katika wachezaji wa Yanga, Papy Tshishimbi ni mfano wa kuigwa kutokana na jinsi anavyomfahamu. Kwasi ambaye aliwahi kucheza na Tshishimbi kwenye kikosi cha Mbabane Swallows ya Swaziland kabla ya msimu uliopita kuibukia Mbao FC, hivi sasa amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Lipuli FC.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kwasi alisema anachofahamu kutoka kwa Tshishimbi ni mchezaji mtulivu ndani na nje ya uwanja, lakini pia anatimiza majukumu yake ya ndani ya uwanja ipasavyo, hivyo ni mchezaji wa kipekee kikosini hapo.
Papy Tshishimbi.
“Namjua sana Tshishimbi kuliko mchezaji mwingine pale Yanga kwa sababu nimewahi kucheza naye kwenye kikosi cha Mbabane, ni mchezaji mzuri kwani anajua anatakiwa kufanya nini na wakati gani ndani ya uwanja.

Kutokana na hilo, naamini ataisaidia sana timu yake, lakini pia ukimkuta nje ya uwanja, ni mtulivu sana hana ile tabia ya ubabeubabe, hivyo ndivyo ninavyomfahamu huyo jamaa,” alisema Kwasi.

Friday, December 29, 2017

Mawingu Tz

Alichokisema Kocha Wa Ndada Kinatisha Jamani Kuhusu Mechi Ya Kesho


KOCHA mkuu wa timu ya Ndanda FC, Malale Hamsini, ametamba kuwa wapinzani wao Simba hawatachomoka katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.
Akizungumza na BINGWA kwa njia ya simu jana kutoka Mtwara, Malale alisema mwaka huu wamedhamiria kukomesha ubabe wa Simba hivyo watahakikisha hawatoki salama ndani ya dakika 90.
“Tumejipanga kushinda, haijalishi tunacheza na timu gani sisi lengo letu ni kupata pointi tatu, hivyo Simba watambue tumejipanga kukabiliana nao na tumedhamiria kushinda katika uwanja wetu wa nyumbani,” alisema.
Aliongeza kuwa mara nyingi wamekuwa wakifungwa na Simba, lakini safari hii wamejipanga kikamilifu kubakiza pointi tatu nyumbani.
Kocha huyo pia aliwamwagia sifa wachezaji watatu waliosajiliwa katika dirisha dogo ambao ni Mrisho Ngassa, Ame Ally na Salum Telela, huku akitamba kuwa nyota hao ndio watakuwa silaha za kumwangamiza mnyama Simba.
“Ngassa na Telela wapo vizuri sana, nitawatumia kama silaha katika mchezo dhidi ya Simba, Ame alichelewa kuripoti kambini hivyo sitamtumia katika mechi hiyo,” aliongeza Malale.
Akielezea kuhusu wachezaji wengine wa kikosi hicho, Malale alisema wapo fiti hivyo kazi aliyonayo ni kutafuta mbinu za kupanga kikosi bora ili waweze kutimiza malengo ya kuvuna pointi tatu muhimu dhidi ya Wekundu hao wa Msimbazi.
Aliongeza kuwa matokeo ya ushindi yatawaweka katika mazingira salama zaidi kwenye msimu wa Ligi Kuu ambapo sasa wanashika nafasi ya 11 baada ya kujikusanyia pointi 11.