Monday, December 11, 2017

Mawingu Tz

Neymar Na Real Madrid Kimeeleweka Tayari

Real Madrid wamefikia makubaliano na Neymar kujiunga na klabu hiyo ya Hispania mwishoni mwa msimu ujao
Mbrazili huyo amekuwa mchezaji ghali zaidi duniani majira ya joto msimu huu baada ya kuhamia Paris Saint-Germain kutoka Barcelona kwa ada ya uhamisho ya £200m.
Licha ya kuikanyaga ardhi akiitumikia PSG, akiwa na magoli 15 na pasi 11 za goli katika mechi 18 tu, tetesi zimeibuka zikidai kuwa Neymar hana furaha kamili katika mazingira yake mapya.
Ripoti kutoka kwenye chanzo cha Hispania Diario Gol zimedai kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amekubaliana na Real Madrid na anatarajiwa kutua Bernabeu mwisho wa msimu wa 2018-19.
Neymar anatamani sana kushinda tuzo ya Ballon d’Or na anaamini kuwa atakuwa na nafasi nzuri kutimiza ndoto zake akiwa katika jiji kuu la Hispania.
Manchester United na Manchester City pia inasemekana zinavutiwana mchezaji huyo, ambaye mkataba wake Parc des Princes utafika ukomo mwaka 2022.

Tupe Maoni Yako