Friday, December 8, 2017

Mawingu Tz

Usajili Unanoga, Toto Africans Yavuta Majembe Sita

Katika kuhakikisha hawashuki kwenda daraja la pili, toto africans imesajili majembe sita ambayo wanaamini yatawasaidia kuondoka kwenye hatari ya kushuka daraja kutoka daraja la kwanza.
Meneja wa timu hiyo, Seleman Abdallah alisema wameanza na wachezaji sita kwanza ambao watakisaidia kikosi chao katika michezo iliyobaki ya mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la Kwanza ingawa matarajio yao nikusajili wacheza kumi.
Abdallah aliwataja wachezaji waliowasajili mpaka sasa kuwa ni Khamis Msafiri, Frank Kimath, Madinda Ramadhan, Henry Shindika, Hassan Dumbu na Ayoub Seleman na bado wanafukuzia wengine.
"Kiukweli  ligi ni ngumu kwa hiyo tumeamua kusajili wachezaji wengi ili waongeze nguvu kwani matarajio yetu ni kufanya vema katika mzunguko wa pili wa daraja la kwanza msimu.”

Tupe Maoni Yako