Friday, December 8, 2017

Mawingu Tz

Himid Mao afunguka kipigo Kili Stars

Nahodha wa Kilimanjaro Stars Himid Mao ‘Ninja’ amezungumzia kipigo cha bao 2-1 ilichopata timu yake kutoka kwa Zanzibar Heroes kwenye michuano ya kombe la Chalenji nchini Kenya kwa kusema kwamba, umakini mdogo ndio uliowapnza.
Baada ya kipigo hicho, Himid amesema Kilimanjaro Stars inatakiwa kupambana ili kushinda mechi mbili za mwisho zilizobaki ili ijiweke kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali.
“Mchezo ulikuwa na ushindani, tulitawala asilimia kubwa ya mchezo lakin dakika za mwisho tulipoteza umakini na kuruhusu magoli.”
“Si dhani kama Zanzibar walitupa tabu, tulifanya makosa mepesi sana ndio yaliyotugharimu sidhani kama kingine kilichofanya watufunge, timu nzima hatuku-defend vizuri. Tunatakiwa kupambana kushinda mechi zinazofuata.”
Kilimanjaro Stars imebakiza mechi mbili kwenye Kundi A dhidi ya wenyeji Kenya na mchezo mwingine utakuwa dhidi ya Rwanda, endapo itashinda mechi hizo itafikisha pointi saba huku ikitegemea pia matokeo ya timu nyingine. Kila kundi zitafuzu timu mbili zenye pointi nyingi kucheza nusu fainali ya kombe la Chalenji 2017.

Tupe Maoni Yako