Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma amemtaka kiungo Haruna Niyonzima kuhakikisha amepona kabla ya kuanza mazoezi rasmi.
Djuma alimuita Niyonzima na kumuweka chini wakati Simba ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterans jijini Dar es Salaam, leo.
Baada ya hapo alimshauri kuacha haraka ya kuanza mazoezi na badala yake kuhakikisha amepona kabisa kabla ya kuanza mazoezi.
Djuma alimueleza Niyonzima kuhakikisha amepona kwa kuwa kama ataanza mazoezi bado akiwa na majeraha anaweza kujisababishia majeraha ya muda mrefu.
Niyonzima alianza kupasha leo lakini inaelezwa hakuwa amepona vizuri lakini kiungo huyo amekuwa na hamu ya kurejea kikosini na kuisaidia timu yake.
Tupe Maoni Yako