Wednesday, December 20, 2017

Mawingu Tz

Umesikia Alichosema Tshishimbi?Kinatishia Furaha Ya Wapinzani Wa Yanga


SI unakumbuka ule moto alioanza nao kiungo fundi wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi, hasa kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba? Sasa jamaa amerudi na makali zaidi ya yale unaambiwa.
Tshishimbi alilazimika kukosa baadhi ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, kutokana na majeraha aliyokuwa nayo lakini sasa amerejea kijeshi kuokoa jahazi.
Kiungo huyo ambaye baada ya kupata majeraha aliondoka kwenda kwao Congo kwa ajili ya matibabu, alizua hofu miongoni mwa mashabiki lakini kuanza kwake kujifua kumeshusha presha.
Katika baadhi ya michezo hiyo ambayo Tshishimbi aliikosa, Yanga ilionekana dhahiri kuyumba eneo la katikati huku timu ikishinda kwa taabu sana.
Kwa sasa Tshishimbi ameanza kujifua huku akionekana kuwa na morali ya hali ya juu hali inayotoa ujumbe kwa mashabiki wao kwamba wakae mkao wa furaha.


Tupe Maoni Yako