Sunday, December 10, 2017

Mawingu Tz

Ukweli Wa Tetesi Wa Ngoma Kutimkia Singida United Wenyewe Wasema Haya

Ukweli wa tetesi wa Ngoma kutimkia Singida United wenyewe wasema haya
Baada ya kuwepo taarifa nyingi zikimhusisha Donald Ngoma kufungashiwa virago ndani ya Klabu ya Yanga hasa kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu wa mara kwa mara klabuni hapo ziliibuka tetesi kuwa huenda Ngoma akajiunga na Singida United.
Ngoma alihusishwa kwenda Singida United kwa kocha wake wa Zamani Hans Van Pluijm ambaye aliwahi kumfundisha wakiwa Yanga kwa mafanikio makubwa.

Baada ya uwepo wa Taarifa Hizi kwataunit.com tulimtafuta Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga ili kujua ukweli juu ya tetesi hizi na Sanga alisema kuwa wao kama Singida United wakati huu wa Dirisha dogo wameongeza wachezaji watatu pekee na wote ni wachezaji wa ndani na siyo wa kimataifa.
Kwa kauli hiyo ni wazi Singida United hawana mpango na Donald Ngoma Mchezaji wa Yanga ambaye mwaka huu aliingia mkataba wa Miaka 2.
Singida United wakati huu wa Dirisha dogo imewaacha wachezaji wawili Atupele Green na Pastory Athanas huku ikiwatoa wawili wengine kwa Mkopo.

Tupe Maoni Yako