Thursday, December 7, 2017

Mawingu Tz

Stand Utd yasajili washambuliaji Kutoka Simba, Singida Utd


Stand United imeendelea kujimalisha kwa kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Simba na Mbeya City, Abdalah Juma.
Stand United yenye maskani yake mjini Shinyanga limefanikiwa kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Singida United, Frank Zakaria.
Stand United imekuwa na tatizo kubwa katika safu yake ya ushambuliaji katika mechi 11 wamekufunga mabao matatu pekee.
Kocha Msaidizi wa kikosi hicho, Agustino Malindi alisema ujio wa mshambuliaji Abdalah Juma na Frank Zakaria kutaisadia kuboresha safu ya ushambuliaji.
Malindi alisema tatizo kubwa kwao msimu huu lilikuwa kwenye safu ya ushambuliaji ambayo ilikuwa butu na kufanya wafunge mabao matatu pekee kwenye mechi 11 za Ligi.
“Sisi tatizo letu kubwa kwenye kikosi chetu ni safu ya ushambuliaji ndio maana umeona tumesajili washambulijia wanne kwa mpigo,” alisema Malindi.
Kocha huyo alijitapa kuwa Stand haweza kushuka daraja msimu ujao kwani wao benchi la ufundi wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanarekebisha kasoro ndani ya kikosi chao.

Tupe Maoni Yako