Sunday, December 10, 2017

Mawingu Tz

Simba Yaweka Wazi Siku Ya Kurejea Kwa Omog.

Kocha Mkuu wa Simba Joseph Omog anatarajiwa kurejea nchini wiki Ijayo tayari kuendelea kukinoa kikosi cha Simba huku akisaidiana na kocha Msaidizi Masoud Djuma
Akizungumza na Simba App Meneja wa kikosi cha Simba Robert Richard alisema ‘Kocha Mkuu anatarajiwa kurejea nchini wiki ijayo ambapo tunatarajia tarehe 14 atakuwa amerejea akitokea nchini Kwao ambapo alikwenda kwenye mapumziko mafupi’
Kocha Omog alisafiri kuelekea Younde Cameroune tarehe 4.11.2017 kwa ajili ya mapumziko mafupi.

Tupe Maoni Yako