Sunday, December 10, 2017

Mawingu Tz

TANZIA: Aliyekua Katibu Wa Yanga Na Mwenyekiti Msidizi TFF Afariki Dunia.

Aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) enzi za FAT (Chama cha Soka Tanzania), Mohammed Misanga amefariki dunia leo akiwa ana umri wa miaka 72
Misanga, Mbunge wa zamani wa jimbo la Singida Kusini (CCM), amefariki dunia katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
Misanga aliyezaliwa Macchi 15, mwaka 1945 amekuwa Mbunge wa Singida Kusini tangu mwaka 2010 na awali mbali ya kuwa kiongozi wa FAT alikuwa pia Katibu wa Yanga SC.
Misanga alikuwa Katibu mkuu wa Yanga wakati inaingia kwenye mgogoro mkubwa wa kihistoria mwaka 1976 uliosababisha klabu kukatika vipande na baadaye kuzaliwa Pan Africa.
Na Misanga ndiye aliyetangaza kufukuza kwa wachezaji waandamizi wote wakiwemo akina Leodegar Tenga, Omar Kapera, Juma Pondamali, Mohamed ‘Adolf’ Rishard na wengineo.
Mungu aipumzishe kwa amani roho ya marehemu. Amin.

Tupe Maoni Yako