Sunday, December 10, 2017

Mawingu Tz

Hatimae Humud Amepata Timu Mpya

Abdulhalim Humud ambaye ni kiungo wa zamani wa Simba na timu ya taifa, Taifa Stars pampoja na Adam Kingwande wamesajiliwa katika timu ya KMC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.
Humud ambaye alikuwa akiichezea Majimaji ya Songea mara ya mwisho anajiunga na KMC katika usajili huu wa dirisha dogo baada ya kutokuwa na timu tangu alipovunja mkataba wake Majimaji na kuondoka.
Kwa siku kadhaa zilizopita mchezaji huyo amekuwa akifanya mazoezi ya pamoja na wachezaji wa KMC kwenye Uwanja wa Bora uliopo Kijitonyama Mabatini jijini Dar es Salaam.


Tupe Maoni Yako