Monday, December 11, 2017

Mawingu Tz

Taarifa Mpya Kwa Mashabiki Wa Simba Kuhusu Golikipa Nduda

Goli kipa wa Simba, Said Mohamed ‘Nduda’, ameanza mazoezi binafsi
kujiweka sawa ili kurejea dimbani baada ya kuwa nje kwa muda mrefu akisumbuliwa na majeraha ya goti.

Nduda aliyesajiliwa na Simba akitokea Mtibwa Sugar baada ya kuonyesha kiwango kwenye michuano ya Cosafa na kuibuka
kipa bora, hajacheza mechi hata moja tangu ametua kwa
Wekundu wa Msimbazi hao kutokana na majeraha hayo ya
goti, lakini baada ya kwenda
kufanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini ameanza kujiweka
sawa.

Majeruhi ya Nduda yaliiweka Simba kwenye wakati mgumu na kuanza kusaka mlinda mlango mwingine ili kushirikiana na kipa namba moja, Aishi Manula na
Emmanuel Mseja, hivyo kuanza
kwake mazoezi kunaweza
kukabadili mpango wa klabu
hiyo kutafuta mbadala wa kipa
huyo.

Akithibitisha hilo, Nduda alisema ameanza mazoezi ya ufukweni kutokana na maelekezo ya daktari na
anatarajia kurejea uwanjani rasmi Januari mwakani.

“Naendelea vizuri nimeanza mazoezi ya peke yangu ufukweni, lakini natarajia kurejea uwanjani rasmi Januari mwakani kwa mujibu
wa maelekezo niliyopewa na daktari,” alisema Nduda.

Tupe Maoni Yako