Monday, December 11, 2017

Mawingu Tz

Yanga Yanasa Straika Hatari Wa Benini..Ni Yule Aliyeitesa Taifa Starz


Klabu ya Yanga kwa mujibu wa gazeti la Dimba la Jumapili inadaiwa wapo katika mipango ya kumnasa Straika wa timu ya Taifa ya Benin Marcelin Koupko.
Taarifa za Uhakika zinasema kuna kiongozi Mkubwa Ndani ya Yanga anafanya mawasiliano na Straika huyo ili kukamilisha dili kabla ya tarehe ya dirisha Dogo kufungwa

Marcelin Koupko anakumbukwa vyema na walinzi wa Taifa Stars wakati wa mchezo wa kirafiki kati ya Benin na Tanzania uliofanyika nchini Benin kutokana na kuisumbua sana Ngome ya Stars.
Endapo Yanga watafanikiwa kumnasa Straika huyo msomaji wa  Chandimu basi huenda njia ya Donald Ngoma ikawa nyeupe kuondoka kutokana na tabia yake ya Utomvu wa Nidhamu.
Taarifa zaidi zinasema Yanga wameshindwa kufanya maamuzi juu ya Ngoma kusubiri kwanza mpaka wapate mbadala wake.

Tupe Maoni Yako