Saturday, December 9, 2017

Mawingu Tz

Lwandamina Awawekea Ngumu Maka Na Muhilu.

Mbao FC iliwahitaji kwa mkopo mshambuliaji Yusuph Mhilu na kiungo Maka Edward ili kuongeza nguvu kwenye kikosi chake.
Hata hivyo habari za uhakika ni kwamba kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina amegoma kuwatoa wachezaji hao kwani amesema atawahitaji kwenye baadhi ya michezo.
Mchezaji pekee aliyepewa ruhusa ya kuondoka kwa mkopo ni Matheo Antony ambaye anaweza kutimkia Kagera Sugar.
Dirisha dogo la usajili linatarajiwa kufungwa wiki ijayo, Disemba 15. Tayari Yanga imesajili wachezaji wawili, Fiston Kayembe Kanku na Yohana Mkomola.

Tupe Maoni Yako