Saturday, December 9, 2017

Mawingu Tz

Tazama:Ratiba Ya Msiba Wa Dk Joel Bendera Leo Jumamosi (Kuaga) Na Kesho Jumapili (Mazishi)

Leo Jumamosi Desemba 9, 2017 ni siku ya kuaga mwili wa mpendwa wetu, Joel Nkaya Bendera - Kocha wa mpira wa miguu wa timu ya Tanzania - Taifa Stars; Mkufunzi wa Makocha wa madaraja ya juu; Mbunge wa Korogwe (Mstaafu); Naibu Waziri wa Michezo (Mstaafu); Mkuu wa Mkoa mstaafu (Morogoro/Manyara) na Mjumbe wa Baraza la Wadhamini TFF.
Shughuli/matukio yatakuwa ni kama ifuatavyo

1. Kifungua kinywa (saa 1.30 hadi 2.00 asubuhi) nyumbani Sinza Mori.
2. Misa hapo hapo nyumbani kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 3.00 asubuhi.
3. Baada ya misa, ndugu, jamaa na marafiki watakwenda Lugalo (kambi ya jeshi) ambako kutakuwa na misa fupi nyingine inayoanza saa 3.30 asubuhi mpaka saa 5.00 asubuhi.

4. Shughuli ya kuaga mwili wa marehemu itaanza mara baada ya misa na itakwnda angalau mpaka saa 7 mchana

5. Safari ya kwenda Manundu, Korogwe mkoani Tanga itaanza mara baada ya shughuli ya kumuaga mpendwa wetu.

Msafara mzima unatarajiwa kuwasili Korogwe jioni ya leo kwa baraka za Mwenyezi Mungu.

Kesho Jumapili Desemba 10, 2017. Tanga

1. Saa 1.30 - 2.30 asubuhi: Kifungua kinywa.

2. Saa 2.30 - 5.00 asubuhi: Maombolezo na kupokea wageni mbalimbali nyumbani kwa marehemu.

3. Saa 5.30 asubuhi - 6.30 mchana: Chakula cha mchana - nyumbani kwa marehemu.

4. Saa 7.00 - 8.30 mchana: Ibada fupi na kuaga nyumbani kwa marehemu.

5. Saa 8.30 - 9.30 Misa ya mazishi katika Kanisa la Mtakatifu Michael.

6. Saa 10.00 kusomwa Historia ya marehemu na mazishi katika Makaburi ya hapo Manundu, Korogwe mkoani Tanga.

Tupe Maoni Yako