Wednesday, December 20, 2017

Mawingu Tz

Juuko Kimeeleweka Simba...Mzamiru,Kichuya Badoo,Vipi Wanasepa Au? Majibu Haya


SASA mashabiki wa Simba wanaweza kushusha presha zao baada ya beki wao kisiki Mganda Jjuuko Murushid, kusaini mkataba mpya wa miaka miwili huku Mzamiru Yasin na Shiza Kichuya wao wakisubiri.
Mmoja wa marafiki wa karibu na Jjuuko amelihakikishia DIMBA Jumatano kwamba, beki huyo pamoja na kiungo mshambuliaji Mohammed Ibrahim ‘Mo’ wameongezewa mikataba na sasa ni mali ya Simba.
Alisema suala la wachezaji hao lilifanyika kimya kimya chini ya Bilionea Mohammed Dewji `Mo`,ambapo mkutano mkuu uliofanyika hivi karibuni uliidhinisha kukabidhiwa klabu hiyo kama mwekezaji.
“Si hao tu pia kuna Mzamiru Yassin na Shiza Kichuya muda wowote kuanzia leo (jana) wataongezewa mikataba mipya kwani hii ya sasa inaelekea ukingoni,” alisema rafiki huyo.
Jjuuko ni miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa wakitajwa mara kwa mara kuungana na Yanga, huku ikidaiwa aliwahi kufanya mazungumzo na mwenyekiti wa kamati ya usajili ya mahasimu wao hao, Hussein Nyika nchini Uganda.

Tupe Maoni Yako