Monday, December 4, 2017

Mawingu Tz

Huyu Msuva Noma Jamani....Azungumzia Misosi Ya Kiarabu

MTANZANIA Simon Msuva anayekipiga klabu ya Difaa El Jadida ya nchini Morocco, jana ameifungia bao klabu yake hiyo katika ushindi wa 4-1 walioupata mbele ya Khouribga na amesema, kwa sasa hana wasiwasi na msosi wa Kiharabu ameshauzoea.
Msuva ambaye ni tegemeo kwenye kikosi cha timu ya Taifa Stars, tangu ajiunge na Difaa El Jadida amekuwa tegemeo kutokana na uhodari wake wa kutengeneza pasi na kufunga mabao.
Katika mchezo huo, Msuva alifunga bao moja na mwenzake, Hamis Ahadad akifunga matatu peke yake.
Akizungumzia chakula, Msuva amesema, awali vyakula vya Morocco vilikuwa vinampa tabu kwa sababu vinatofautiana kimapishi na vya Tanzania.
"Chakula ni kile kile tu, utofauti wao ni katika mapishi. Mwanzoni nilianza kwa shida lakini sasa nazoea, ujue kitu ukikizoea alafu ikatokea ukiache na kuanza upya inahitaji muda ndivyo ilivyokuwa kwangu,” anasema Msuva.

Tupe Maoni Yako