Friday, December 8, 2017

Mawingu Tz

Hii Ni Taarifa Mbaya Kwa Mashabiki Wa Yanga Kuhusu Yondani

Beki kisiki wa klabu ya Yanga, Kelvin Yondani atalazimika kukaa nje kwa takribani majuma mawili kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu aliyopata jana akiitumikia timu ya taifa ya Tanzania Bara(Kilimanjaro Stars).
Kwa mujibu wa Daktari wa timu ya Tanzania Bara,DR.Richard Yomba amesema tayari Yondani ameanza matibabu na atarejea dimbani baada ya wiki mbili.
Hivyo huenda akaukosa mchezo wa kombe la FA dhidi ya Reha utakaopigwa kati ya December 20 na 25.

Tupe Maoni Yako