Friday, December 22, 2017

Mawingu Tz

Simba Kuanza Kuutetea Ubingwa Wa FA Leo..Kuwakosa Wachezaji Hawa Wanne

Vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba leo wataanza kutetea ubingwa wake wa Kombe la FA kwa kuivaa Green Warriors bila ya nyota wake wa kimataifa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamanzi.


Simba inayachukulia mashindano hayo kwa uzito mkubwa kwani ndiyo yaliyowapa nafasi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani baada ya kuifunga Mbao FC kwa mabao 2-1 katika fainali iliyofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma msimu uliopita.

Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog alisema watakaokosekana Mganda Emmanuel Okwi, Waghana James Kotei na Nicholas Gyan wenye matatizo ya kifamilia, huku Haruna Niyonzima akiwa ni majeruhi.

Omog alisema katika wachezaji wa kigeni atakayecheza mechi hiyo ni beki Juuko Murshid.

Katika mazoezi ya jana asubuhi kwenye Uwanja wa Boko Veterans, kiungo Haruna Niyonzima alipewa mazoezi ya peke yake na daktari wa timu hiyo Yassin Gembe.

"Naendelea vizuri na matatibu natakiwa kufanya mazoezi peke yangu huku daktari akiniangalia, naimani sitaweza kucheza mechi ya FA, ila ile ya Ndanda naweza kuiwahi," alisema Niyonzima.

Katika kuhakikisha wanakuwa vizuri kila idara kocha huyo aliwapa wachezaji wake mazoezi ya kupiga penalti

Kocha Omog baada ya kuwapigisha tizi wachezaji wake katika uwanja huo wa Boko aliwapa zoezi la kupiga penalti na aliyekuwa akikosa alimtenga na waliopata na alifichua anawaandaa wachezaji kwa mechi hiyo ya leo.

Omog alisema mechi hizi za FA, ni za mtoano na kama dakika 90 zitaisha kwa sare, lazima wapigiane penalti hivyo anawaandaa mapema vijana wake.

Tupe Maoni Yako