Friday, December 22, 2017

Mawingu Tz

Simba Noma Sana Kimataifa..Watuma Ujumbe Mzito CAF


UKISEMA Simba wametuma ujumbe kwa Shirikisho la Soka Afrika (Caf), utakuwa sahihi na hii ni baada ya kusema wanataka kufanya kila linalowezekana kutwaa ubingwa wa michuano yote iliyopo mbele yao ikiwamo Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Ujumbe huo walioutuma Simba, pia ni kama unawalenga wapinzani wao wa jadi Yanga, ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Wekundu wa Msimbazi hao wamesema lazima ubingwa utue kwao ikiwamo pia kutetea ubingwa wa Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC).
Katika michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, Simba wataanza kucheza dhidi ya Endarmerie ya nchini Djibouti na wakifanikiwa kuvuka watakutana na mshindi kati ya Al-Massry ya nchini Misri dhidi ya Green Buffaloes ya Zambia.

Tupe Maoni Yako