Wednesday, December 20, 2017

Mawingu Tz

MPYA:Habari Mpya 2 Kutoka Yanga Leo December 20,2017

RATIBA YA MAZOEZI
Baada ya jana Kufanya mazoezi ya gym klabu ya Yanga leo inatarajiwa kuendelea na mazoezi ya uwanjani KATIKA uwanja wa Uhuru wakiongozwa na Kocha Mkuu George Lwandamina.
Yanga inajiandaa na Mchezo wa kombe la Shirikisho wikiendi hii na mchezo wa Ligi kuu ambao watalazimika kusafiri mpaka jiji la Miamba Mwanza Kuifata Mbao Fc.
KAMUSOKO TARATIBU ANAENDELEA POA
Kiungo wa timu ya Yanga Mzimbabwe Rasta Thaban Kamusoko taarifa zinaeleza kuwa ameanza kuwa fiti na tayari anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi mara baada ya kufanyiwa matibabu ya kitaalamu zaidi kwenye Goti lake ambalo limekuwa likimsumbua.
Kamusoko ambaye amekaa nje kwenye kikosi cha Yanga takribani miezi miwili kupona kwake na kuwa fiti kutaimarisha zaidi eneo la kiungo cha Yanga.

Tupe Maoni Yako