Saturday, December 23, 2017

Mawingu Tz

KIMEELEWEKA:Maamuzi Ya Mwisho Kuhusu Ishu Ya Asante Kwasi Haya Hapa

Mara baada ya Simba kuwaandikia barua timu ya Lipuli Fc kutoka mkoani Iringa na Lipuli kuthibitisha kupokea Barua ya Lipuli na kuwataka Simba waende Mezani kujadili na kuangalia namna ya kumaliza suala hilo kwani Simba walithibitisha kumwitaji mchezaji huyo ambaye alikuwa bado na mkataba wa miezi 8 Lipuli.
Jana mwenyekiti wa Lipuli Ramadhani Mahano ameiambia kwataunit.com kuwa wameshamalizana na Simba na kwasasa Asante Kwasi ni mchezaji halali wa Simba baada ya kila kitu kukaa sawa.
” Tumemalizana na Simba baada ya kufanya mazungumzo viongozi wa pande zote mbili na kwasasa Kwasi sim mchezaji wetu tena, ni mchezaji wa Simba na tunawakaribisha tena Simba kama wakitaka mchezaji mwingine “

alimaliza Mahano ambaye aliongea kwa furaha tofauti na siku kadhaa alipokuwa akiripoti Simba kutaka kuwazunguka kwenye suala la kumsajili Asante Kwasi, FUraha hiyo illionekana wazi kiasi cha Kiongozi huyo kuwakaribisha tena Simba watakapotaka mchezaji.
Kwasi msomaji wa Kwataunit alitikisa vyombo vya habari kuhusiana na usajili wake Simba , Na hii ilikuja kuwa kubwa zaidi mara baada ya Simba kuonekana wakimsaini mchezaji huyo hali iliyofanya viongozi wa Simba kuwa na Kigugumizi kuhusiana na Suala hilo.
Lakini kwa baadaye Simba kupitia kwa Mwenyekiti wa kamati ya Usajili ZACHARIA HANSPOPPE alikiri kuwaandikia barua Lipuli juu ya kumwitaji mchezaji na Viongozi walipozungumza mambo yameisha kwa Lipuli kufuta jina la Asante KWASI na mchezji huyo kusajiliwa Simba Rasmi.

Tupe Maoni Yako