ISHU YA TSHISHIMBI KUMPIGA MCHEZAJI MWENZIE NGUMI HII HAPA
Ilikuwa ni katika mazoezi ya Yanga jana yanayofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar Es Salaam ndipo tukio zima lilipotokea.
Tshishimbi alikuwa na Mpira akijipanga kutafuta mchezaji wa kumpa pasi na ndipo katika hali ambayo siyo ya kawaida kinda wa Yanga Seleman Yusuph anayecheza timu ya Vijana ya Yanga alimvaa Tshishimbi na kumchezea Faulo.
Tshishimbi akaamua kumpiga ngumi ya kishkaji kama kumtahadharisha kijana huyo kwani kiungo huyo raia wa Congo ametoka kwenye majeraha hivyo aliona kama dogo anataka kumrudisha alipotoka.
Na alipotafutwa Seleman Yusuph baada ya mazoezi alisema kuwa hajachukia kupigwa Ngumi na Tshishimbi kwani ndiyo mambo ya soka hayo na kusema yeye (Tshishimbi) alichomaindi ni kuingiliwa vibaya hali ambayo kwenye mpira hutokea wakati wowote.
Yanga wapo katika mazoezi makali wakijiandaa na mchezo dhidi ya Reha inayoshiriki ligi daraja la Pili, Mechi hiyo itapigwa siku ya Jumapili katika uwanja wa Uhuru jijini Dar Es Salaam.
Wakati huo watani wao Simba watakuwa na mchezo leo jioni dhdi ya Green Warriors Kwataunit.com tutakupa kila taarifa kuelekea mchezo huo na mingine yote,
Tupe Maoni Yako