Monday, December 4, 2017

Mawingu Tz

Eeeh Bwana Unaambiwa Kichuya Sio Tu Mkali Wa Mabao Uwanjani....Na Huku Nako Mkali

HUYO Shiza Kichuya achana naye. Mshambuliaji huyo wa Simba, kumbe si mkali wa mabao tu, hadi kwenye uwekezaji nako anapiga mabao.
Kwa Kichuya kila mkwanja anaovuta, unatumika ipasavyo katika uwekezaji.
Kichuya aliyeifungia Simba mabao 17 ya Ligi Kuu Bara tangu alipojiunga nayo msimu uliopita, mpaka sasa anamiliki viwanja viwili na nyumba, vyote vikiwa katika Manispaa ya Morogoro.
Kwa mujibu wa Meneja wake, Profesa Midundo Mtambo, dau la usajili alilopata Simba, lilitumika kununulia viwanja hivyo huku akinunua nyumba kwa fedha zake nyingine.
“Hizo ndizo mali za Kichuya, ila naamini ipo siku atakuwa mbali zaidi, kwani ni mtu anayependa kuwekeza kuliko kufanya starehe, mfano mzuri ni pale aliponunua nyumba kwa shuguli zake nje ya soka,” alisema.
Alisema kwa aina ya uchezaji wake, anaamini anaweza akabadilisha maisha kupitia kipaji cha soka, huku akimfunda asije akakengeuka nakujiona anajua kila kitu.
“Kila kitu ni hatua, kwa sasa hana gari licha ya jina lake kuwa maarufu, ila namshauri juhudi na kutokata tamaa ndio silaha ya maisha yake, ni mfano kwa jamii inayomzunguka,” alisema.
Lakini kuhusiana na msimamo wake juu ya wapi Kichuya atasaini na dau lake litakuwa kiasi gani, meneja hiyo alisisitiza kusubiri mkataba wa sasa umalizike kabisa ndipo watachagua timu itakayomnufaisha.
“Vuta subra, kuna timu zinazohitaji huduma yake, za ndani na nje pia, lakini kwa sasa nimemwambie azidi ndiyo silaha ya mafanikio,” alisema.

Tupe Maoni Yako