Saturday, December 23, 2017

Mawingu Tz

Alichokisema John Bocco Baada Ya Simba Kutupwa Nje Azam Sports Federation Cup.

Nahodha wa kikosi cha timu ya soka ya Simba SC ya Jijini Dar es Salaam John Raphael Bocco amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo kwa kushindwa kuifunga Green Warriors na kusonga mbele katika michuano ya Azam Sports Federation Cup.
Bocco amesema kupoteza kwenye mchezo huo halikuwa tegemeo lao kwani waliamini kabisa kuwa wataibuka na ushindi ukizingatia mpinzani waliyepangwa naye.
-Matokeo haya hatujayafurahia kwa sababu haikuwa mipango yetu, tulijiandaa tushinde, ukizingatia na timu ambayo tulikuwa tunacheza nayo ya daraja la pili lakini kwa yote tunamshukuru Mungu, mpira ni mchezo wa makosa wenzetu wameweza kuyatumia,” amesema Bocco.
John Bocco ambaye amejiunga na timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu amesema wanachoangalia sasa ni michezo iliyombele yao ambapo watajitahidi kuhakikisha wanashinda ili kuwafuta machozi mashabiki wa timu hiyo popote walipo.
-Saa nyingine mpira hutokea kama hivi, kikubwa tunaangalia makosa yetu, tunaenda kujifunza ili pale tulipokosea tufanye vizuri katika mechi zinazofuata,” ameeleza.

Tupe Maoni Yako