Tuesday, November 28, 2017

Mawingu Tz

Wachezaji Tp Mazembe Wazawadia Milioni 11 Kila Mmoja

Baada ya Mabingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika, TP Mazembe kubeba taji hilo, neema imeendelea kuwatawala ambapo safari hii wamepata mzigo kutoka kwa Waziri wa Michezo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Papy Nyango.
Klabu hiyo imekabidhiwa kitita cha dola 5,000 za Kimarekani kwa kila mchezaji wa kikosi hicho walioipeperusha vema bendera ya taifa hilo nchini Afrika Kusini walipowafunga Super Sport katika fainali. Kiasi hicho cha fedha ni sawa na zaidi ya Sh milioni 11 kwa kila mchezaji.
Kitita hicho kutoka Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupitia kwa Waziri huyo wa Michezo kinatajwa kuwa kama motisha kwa wachezaji hao na kuthamini mchango wa jasho lao mbele ya bendera ya Congo.

Tupe Maoni Yako