Tuesday, November 28, 2017

Mawingu Tz

Ronaldo Akasirishwa Na Mkataba Mpya Wa Lionel Messi

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo imeripotiwa kuwa na "ghadhabu" juu ya mkataba wa mpya wa Lionel Messi na Barcelona.
Baada ya miezi ya tetesi, juzi Jumamosi, Messi alisaini mkataba mpya utakaombakiza Camp Nou hadi mwaka 2021.
Messi mwenye umri wa miaka 30 sasa imeripotiwa kuwa amesaini mkataba mnono wenye thamani ya pauni 626m na mshahara wake kuongezeka hadi pauni 525,000 kwa wiki sawa na pauni 90m katika kipindi chote cha mkataba wake.
Kiasi hicho kinampa Messi ujira wa takribani 50% juu zaidi ya Ronaldo, ambaye inaaminika analipwa pauni 360,000 kwa wiki na Los Blancos.
Inadaiwa kuwa Ronaldo "alilipuka kwa hasira" aliposikia habari za mkataba mpya wa Messi kwani ameshindwa kuimarisha mkataba wake binafsi kwa miezi mingi.
Mshambuliaji huyo wa Kireno yupo kwenye mkataba hadi 2021 lakini imeripotiwa kuwa hana furaha na maisha ya jiji la Madrid na alikuwa akihusishwa na tetesi za kutaka kurudi Manchester United majira ya joto.

Tupe Maoni Yako