Thursday, November 30, 2017

Mawingu Tz

Suala La Asante Kwasi Kwenda Simba,Lipuli Wasema Haya

Ikiwa Ni wakati wa Dirisha dogo na baadhi ya timu kuwa tayari zimeanza mchakato wa kuongeza na kupunguza wachezaji ili kuimarisha vikosi vyao, Moja kati ya wachezaji wanaotajwa kutakiwa na Simba ni Asante Kwasi kutoka Timu ya Lipuli ya Iringa.
Klabu ya Lipuli wamefunguka kuhusu tetesi za mchezaji huyo anayetajwa kuwa katika rada za Simba wakati huu wa Dirisha dogo, Mwenyekiti wa klabu ya Lipuli Ramadhan Mahano amesema
MPAKA LEO HAKUNA KLABU ILIYOFANYA MAZUNGUZO YA KUMTAKA MCHEZAJI WA LIPULI, LABDA NISEME TU KAMA KUNA KLABU INAMTAKA MCHEZAJI WA LIPULI BASI IFUATE UTARATIBU KWANI WACHEZAJI WOTE WANAMKATABA,KLABU ZIFUATE UTARATIBU ILI MCHEZAJI NA KLABU WOTE WANUFAIKE
Asante Kwasi msomaji wa Kwataunit.com ni beki lakini mpaka sasa ameshafunga jumla ya magoli matano katika mechi 11 za VPL ambazo zimeshachezwa mpaka sasa.

Tupe Maoni Yako