Thursday, November 30, 2017

Mawingu Tz

Kamusoko Hali Tete Yanga..Yanga Waamua Maamuzi Haya

Uongozi wa Yanga umelazimika kumsafirisha kiungo wake, nahodha msaidizi Thabani Kamusoko nchini India kupata matibabu ya majeraha ya mguu yanayomsumbua kwa wiki kadhaa sasa.
Imeelezwa licha ya matibabu aliyokuwa anapatiwa hali ya mchezaji huyo haijaimarika hivyo kulazimika kumsafirisha nchini India kwa matibabu ya kitaalam zaidi.
Msimu huu Kamusoko ameichezea Yanga michezo miwili pekee kabla hajaanza kusumbuliwa na matatizo ya kisigino.
Yanga imedhamiria kuhakikisha hali za wachezaji wake wote ni timilifu kwenye mzunguuko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom ili kuhakikisha inatetea ubingwa wake kwa msimu wa nne mfululizo.

Tupe Maoni Yako