Friday, December 1, 2017

Mawingu Tz

Straika Hatari Wa Rayon Sports Aigomea Simba Sc..Asema Yeye Sio Wa Level Izo

Wakala wa straika Shasir Nahimana wa Rayon sports amewambia mabosi wa kamati ya Usajili ya Simba kuwa kama wanamtaka mchezaji wake wamsainishe na sio kumuita nchini kumjaribu.
Straika huyo na wenzake wawili waliotajwa kuhitajika katika kikosi cha wanamsimbazi hao ambao kwa sasa wanauhitaji mkubwa wa mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa wa kucheka na nyavu ambae ataweza kusafisha makosa yanayofanywa na washambuliaji waliopo kwa sasa.
Nahimana na Kelvin Muhere majina yao yalipendekezwa kwenye kamati hiyo ya kocha msaidizi wa Simba kwa kuwa aliwaona kabla ya kutua katika kikosi cha Simba.
Kocha huyo akizungumzia kauli ya wakala wa mchezaji huyo amesema kuwa amesikia taarifa hizo na kuongeza yeye na Kocha mkuu hawawezi kukubaliana na hilo.
“Lakini nasikia kuwa wakala wake anataka kama mchezaji wake atakuja hapa nchini aje kusaini, Sidhani kama mimi na Kocha mkuu tunaweza kukubaliana nalo”. Aliongeza Djuma.

Tupe Maoni Yako