Friday, December 1, 2017

Mawingu Tz

Ngoma Noma Aonekana Mlimani City Akila Bata

HALI ni mbaya kwa straika Mzimbabwe Donald Ngoma ambaye amesharejea Dar es Salaam na leo, alionekana akifanya matanuzi mida ya mchana kwenye kiwanja kimoja ndani ya Mlimani City.
Ngoma ambaye anasifika kwa soka yake nzuri lakini ameikera klabu ya Yanga baada ya kuondoka kwenda kwao Zimbabwe bila ruhusa na sasa wameshatengeneza mpango ya kumleta mbadala wake.
Yanga inafanya mchakato wa kumsajili straika atakayeziba nafasi hiyo na mmoja kati ya Bensua Da Silva kutoka Guinea Bisau mwenye asili ya Ivory Coast, Badara Kella raia wa Sierra Leone na Mghana Adam Zikiru ndiye atakayechukua nafasi.
Lengo la benchi la ufundi ni kupata washambuliaji wa kwanza maalum kwa ufungaji baada ya kupotea kwa Amissi Tambwe anayesumbuliwa na majeraha.
Sababu ya Ngoma kukatwa inadaiwa ni kuondoka kwenda kwao Zimbabwe bila ruhusa ya Yanga na klabu hiyo, imekiri kumlima barua .
Hata hivyo, usajili wa mmoja wa wachezaji hao, utakamilika pale tu atakapolirizisha benchi la ufundi kwenye majaribio.

Tupe Maoni Yako