Friday, December 1, 2017

Mawingu Tz

USAJILI: Yanga Kushusha Wa3 Wa Kimataifa,1 Kumrithi Ngoma,Wafahamu Hapa

Klabu ya Soka ya Yanga inayodhaminiwa na Kampuni inayojihusisha na michezo ya kubahatisha ya SportPesa ni wazi kuwa wanataka kuboresha kikosi chake kabla ya DIRISHA DOGO kufungwa December 15.
Yanga ambao pia wanatajwa kuwa huenda wakamtosa STRAIKA wao Donald Ngoma kutokana kuwa mtomvu wa Nidhamu na tayari kuna Mastraika watatu wa Kimataifa watakuja kwaajili ya Majaribio na Mmoja kati yao ndiye atakayemrithi Donald Ngoma Yanga wakati huu wa Dirisha dogo.
Wachezaji hao wa Kimataifa ni Badara Kella ambaye ni raia wa Sierra Leone, Adam Zikiru kutoka nchini Ghana na Bensua Da Silva kutoka Guinea Bisau mwenye asili ya Ivory Coast.
Kati ya hao watatu mmoja ndiye atakayevaa viatu vya Donald Ngoma ambaye kwasasa ameshatua Nchini viongozi wa Yanga wakisubiri kutoa maamuzi juu yake kutokana na kutuhumiwa kuondoka nchini bila Taarifa.
Boniface Mkwasa ambaye ndiye katibu mkuu wa Yanga ameiambia Chandimu  kuwa tayari Ngoma ameshawasilisha Barua zinazoeleza utetezi wake juu ya kwanini alienda kwao nchini Zimbabwe na Kinachosubiriwa kwasasa ni maamuzi ya Mwisho kutoka kwenye kamati ya Nidhamu ya Klabu hiyo.


Tupe Maoni Yako