Friday, December 1, 2017

Mawingu Tz

Hatimaye Serikali Yakubali Mo Dewji, Manji Wawe Mabosi Simba Na Yanga

WAKATI sakata la uwekezaji likiendelea kuteka hisia za wadau wengi wa soka la nchini Tanzania, hatimaye serikali imetoa tamko juu ya aina ya uwekezaji ambao unatakiwa na ulioruhusiwa.
Hivi karibuni kuliibuka juu ya maamuzi ya uwekezaji ambapo Klabu ya Simba ilikuwa kwenye mchakato wa kufanya mabadiliko ya umiliki na uongozi wa klabu kama ilivyo kwa Yanga.
Inalezwa kuwa mwanachama wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’ anawania nafasi ya kumiliki hisa pindi mabadiliko yatakapofanyika, huku Yanga mtu aliyekuwa akitajwa ni mfanyabiashara Yusuf Manji ambaye alikuwa mwenyekiti wa klabu hiyo.
Akizungumza kwa ufupi kuhusu suala hilo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ametamka kuwa wao serikali wameruhusu uwekezaji na wapo tayari kuona hilo likifanyika.
Amesema pamoja na kukubaliwa lakini mwekezaji mkuu anatakiwa kumiliki hisa zisizozidi asilimia 49 ili kuwapa nafasi wale wamiliki halisi wa klabu kuendelea kuwa na sauti.
Ameongeza kuwa serikali haikatazi uwekezaji lakini hilo linaweza kufanyika kwa kuzingatia kigezo hicho ili kutoondoa umiliki wa klabu hasa zile za wanachama.
Ametolea mfano nchini Ujerumani ambapo mfumo huo unatumika na umekuwa na msaada katika kukuza soka la ndani la nchi hiyo tofauti na Uingereza ambapo mwenye fedha nyingi anamiliki klabu na ndiye anakuwa na sauti.

Tupe Maoni Yako